Posts

Showing posts from June 21, 2018

Wabunge nchini Tanzania hii leo wanafanyiwa vipimo vya virusi vya ukimwi

Wabunge nchini Tanzania hii leo wanafanyiwa vipimo vya virusi vya ukimwi huko mjini Dodoma ikiwa ni jitihada za viongozi hao kuishi kwa mfano katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi. Mbali na vipimo vya hiari, wabunge hao pia watakuwa na shughuli mbali mbali kama njia moja wapo ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kampeni yake ya upimaji virusi vya ukimwi nchi nzima imezinduliwa na Waziri mkuu Kassim Majaaliwa. Kwa mujibu wa takwimu za serikali takriban watu milioni 1.4 wanaishi na virusi vya ukimwi lakini ni asilimia 52 tu walio na ufahamu kuhusu hali zao. Serikali imeidhinisha kampeni ya miezi sita inayonuiwa kuwatibu watu wanaoishi na virusi vya HIV kwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARVs). Zaidi ya wabunge 300 wa Tanzania wanatarajiwa kutoa mfano mwema kwa kujipima hadharani katika makao ya bunge Dodoma. Tayari waziri wa afya nchini Ummy Ali Mwalimu , spika wa bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wametangu...