Canada sasa ruhusa matumizi ya bangi hadharani
Canada sasa ruhusa matumizi ya bangi hadharani
Haki miliki ya picha Getty Images Image
caption Bangi sasa halali Canada
Canada imepitisha sheria rasmi kwa
nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi.
Sheria hiyo hatimaye ilishinda kwa
kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani,huku kura 29
za maseneta zikisema hapana.
Sheria hiyo inasimamia
udhibiti,usambazaji na uuzaji wake.
Haki miliki ya picha AFP/GETTY Image
caption Raia wa Canada wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia
mapema mwezi Septemba
Kwa sheria hiyo sasa raia wa Canada
wataruhusiwa kununua na kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi Septemba
mwaka huu.
Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa
kisheria tangu mwaka 1923 lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa
kisheria tangu mwaka 2001.
Kutokana na kupitishwa kwa sharia
hiyo sasa itawachukua majimbo,Manispaa na mamlaka takribani wiki kati ya nane
hadi 12 kutengeneza masoko mapya ya kuuza bangi.
Lakini pia muda huu kabla ya kuanza
kutumika kwa bangi rasmi,utatumika na Polisi kuandaa mifumo mipya ya kisheria.
Kwa mjibu wa sheria hii mpya mtu
ataruhusiwa kuagiza bidhaa hii ya bangi kwa mfumo wa kimtandao kutoka kwa
wasambazaji wanaotambulika kisheria.
Haki miliki ya picha PRESS
ASSOCIATION Image caption Watu nchini Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa
bangi duniani.
Watu wazima wataruhusiwa kumiliki
hadharani hadi gram 30 ya bangi kavu hadharani.
Umri unaoruhusiwa kununua na kutumia
bangi umepitishwa kwa mjibu wa sharia hiyo kwamba ni kuanzia miaka 18,lakini
baadhi ya majimbo yamependekeza umri wa kuanzia miaka 19. Ni
Ni
kwa nini Canada ifanya hili sasa?
Sheria hiyo inahitimiza ahadi ya
kampeni ya Bw Tudeau, kioongozi wa chama cha Liberal.
Waziri huyo mkuu amesema kuwa sheria
za miaka mingi za Canada zinazoharamisha matumizi ya bangi hazina maana kwa
kuwa watu nchini Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa bangi duniani.
Kura za maoni zimekuwa zikionyesha
kuwa watu wengi nchini Canada wanaunga mkono hatua hiyo.
Hatua ya kuhalalisha matumizi ya
bangi kwa burudani nchini Canada yanakuja wakatoi nchi za dunia zinahalalisha
bangi inayotumiwa kwa kiwango kikubwa duniani.
na mwandishi wako saumu kweka
Comments
Post a Comment