MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA
Msanii wa bongo flavor Salum Mohamed aliyetamba kwa jina la Sam wa ukweli amefariki dunia Usiku wa kuamkia 7,2018 Sam alitamba sana na kazi zake kama vile sina raha ,
alioutoa Mwaka 2010, usiniache loully , hata kwetu wapo
Baada ya ukimya wa muda mrefu alibuka tena mwishoni mwa 2017, na kibao kingine , kwa jina
la kisiki, na mwanzoni mwa mwaka 2018, akauachia wimbo mwingine unaoitwa ni wewe
Ingawa ni mtu wa Singida Sam wa ukweli amekulia kiwangwa
jirani na mji wa Dar es salaam ambako amelelewa na Bibi yake mzaa Mama , kwa
mujibu wa Meneja wake Abdulmalik Mohamed, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hosipitali ya Mwananyamala , jijini Dar es salaam , na mipango ya mazishi inaendelea katika eneo la Tandale, lakini
maziko yatafanyika alhamisi hii kiwangwa mkoani Pwani
Na mwandishi, Tumaini Swai
Comments
Post a Comment