MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA BARABARA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mheshimiwa GABRIELI .F.
DAQARO amefanya ziara yake mkoani hapa
ya kutembelea barabara ya TARURA mijini
na vijijini , ambayo imekuwa ikikarabatiwa kwanzia mwezi wa kwanza mpaka sasa na
ametembelea barabara ya kata za kati, Levolosi , Terati na Murieti.
GABRIEL
DAQARO, amesema kuwa wanatembelea kwasababu ni kazi yao ya kawaida kutembelea miradi hiyo ili kujua kazi
inayoendelea ndani ya wilaya na kazi inaenda vizuri lakini baadhi ya maeneo ni
ya kusisitiza kwasababu kuna maeneo yanalegalega na wanatofautiana na mkataba
waliyo pewa na serikali katika
utengenezaji wa barabara.
Ameendelea
kwa kusema kwamba, kutokana na kampuni ambazo hazijafanya kazi kwa wakati
muwafaka amekubaliana na TARURA kwa
kutaka kazi ziheshimiwe kulingana na mkataba uliowekwa na serikali na kufikia
tarehe 14 mwezi wa nane mwaka huu 2019 kazi iwe imekamilika.
Hata hivyo
amesema kuwa wapo wakandarasi ambao hawaeleweki na sababu wanazotoa ambazo siyo
za msingi na wamesha toa maelekezo kwa TARURA kwa kuhakikisha kwamba
wakandarasi ambao wanayumbayumba watambulike ili kwa kazi ya serikali ijayo
watambulike ili kutokupewa kazi tena.
Vilevile
Mheshimiwa mkuu wa wilaya amesema kuwa kila mwisho wa wiki wakandarasi na
wasimamizi wote wanatakiwa kupeleka taarifa namna gani mradi huo unavyokwenda
kwasababu wapo baadhi ya wakandarasi ambao hawapo site.
Aidha
amesema kuwa wapo wakandarasi ambao hawalipi wafanyakazi wanaofanya zile kazi za muda na ameelekeza
TARURA wagunduwe stahiki za wafanyakazi hao walipwe shilingi elfu kumi (10000)
kwa siku na wahakikishe kuwa watu hao hawanung’uniki,hawanyanyaswi na
hawanyonywi.Na wahakikishe kwa wale wanaosuwasuwa inapo bidi watavunja mkataba nao na waangalie
thamani ya fedha.
Naye kiongozi wa TARURA FODEM MWAKENJA amesema
kuwa maelekezo haliotoa mkuu wa wilaya yatafanyiwa kazi kwa muda uliowekwa na
serikali, na kwa wale wakandarasi ambao hawafati mikataba inasema nini watawachukulia
hatua za kisheria .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe:GABRIELY.F.DAQARRO (katikati) akikagua miongozo ya kazi inayoendelea katika utengenezaji wa barabara ya TARURA mkoani Arusha.
Comments
Post a Comment