Posts

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA BARABARA.

Image
Mkuu wa   wilaya ya Arusha Mheshimiwa GABRIELI .F. DAQARO amefanya ziara yake   mkoani hapa ya kutembelea barabara ya TARURA   mijini na vijijini , ambayo imekuwa ikikarabatiwa kwanzia mwezi wa kwanza mpaka sasa na ametembelea barabara ya kata za kati, Levolosi , Terati na Murieti. GABRIEL DAQARO, amesema kuwa wanatembelea kwasababu ni kazi yao ya   kawaida kutembelea miradi hiyo ili kujua kazi inayoendelea ndani ya wilaya na kazi inaenda vizuri lakini baadhi ya maeneo ni ya kusisitiza kwasababu kuna maeneo yanalegalega na wanatofautiana na mkataba waliyo pewa na serikali   katika utengenezaji wa barabara. Ameendelea kwa kusema kwamba, kutokana na kampuni ambazo hazijafanya kazi kwa wakati muwafaka   amekubaliana na TARURA kwa kutaka kazi ziheshimiwe kulingana na mkataba uliowekwa na serikali na kufikia tarehe 14 mwezi wa nane mwaka huu 2019 kazi iwe imekamilika. Hata hivyo amesema kuwa wapo wakandarasi ambao hawaeleweki na sababu wanazotoa ambaz...

MULIKA-Toleo la Mwezi Septemba 2018

Image

Mmomonyoko wa maadili kwa wanavyuo

Image
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji   The Arusha East African Training Institute wakiwa kwenye semina yenye kichwa   cha somo linalosema   “ mmomonyoko wa maadili unavyoweza kuathiri   taaluma ya mwanachuo au wanachuo” , inayotolewa na Mch wa kimataifa Gift Urio maarufu kwa jina la AK47.                                                      Wanafunzi wa chuo wakiwa wanasikiliza semena                                                      iliyokuwa ikiendeshwa katika eneo la chuo philips                     ...

Wabunge nchini Tanzania hii leo wanafanyiwa vipimo vya virusi vya ukimwi

Wabunge nchini Tanzania hii leo wanafanyiwa vipimo vya virusi vya ukimwi huko mjini Dodoma ikiwa ni jitihada za viongozi hao kuishi kwa mfano katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi. Mbali na vipimo vya hiari, wabunge hao pia watakuwa na shughuli mbali mbali kama njia moja wapo ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kampeni yake ya upimaji virusi vya ukimwi nchi nzima imezinduliwa na Waziri mkuu Kassim Majaaliwa. Kwa mujibu wa takwimu za serikali takriban watu milioni 1.4 wanaishi na virusi vya ukimwi lakini ni asilimia 52 tu walio na ufahamu kuhusu hali zao. Serikali imeidhinisha kampeni ya miezi sita inayonuiwa kuwatibu watu wanaoishi na virusi vya HIV kwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARVs). Zaidi ya wabunge 300 wa Tanzania wanatarajiwa kutoa mfano mwema kwa kujipima hadharani katika makao ya bunge Dodoma. Tayari waziri wa afya nchini Ummy Ali Mwalimu , spika wa bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wametangu...